Elimu ya mtaani na maajabu yake.

Elimu ya mtaani na maajabu yake katika mafanikio ya ndoto za watu.

Elimu ya mtaani,Elimu ya fedha na uchumi

Ndugu msomaji wangu naamini kuwa umzima wa afya popote pale ulipo na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku katika juhudi za kuyajenga mataifa yetu. Yamkini hapo unapoisoma makala hii unatumia mojawapo ya chombo cha mawasiliano kama simu, kompyuta au hata kishikwambi.

Bila kupepesa macho nikupongeze wewe hapo unayeendelea kuyasoma maneno haya kwa kuwa umeamua kuchukua maamuzi sahihi kabisa na kukitumia chombo chako cha mawasiliano si tu kwa kuwatafuta ndugu, jamaa na marafiki bali pia kama darasa huru la kukuongezea maarifa na elimu ya mtaani kwa ujumla.

KUSOMA SIYO WAJIBU WA WANAFUNZI MASHULENI NA VYUONI TU

Elimu ya mtaani,Elimu ya fedha na uchumi

Kipekee ningeomba kutoa wito kwa vijana WOTE  kuachana na dhana ya kuamini kuwa jukumu la kusoma lipo tu kwa wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni laa hasha bali watu wote hasa vijana tunatakiwa kupenda kusoma vitabu, majarida, makala mbali mbali, nk. Kwani kwa kusoma mara kwa mara tutajifunza mambo mengi yatakayotuwezesha kuyakabili matatizo na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye maisha yetu ya kila siku. Japokuwa limekuwa ni suala gumu kwa vijana wengi kujikita katika kusoma mambo yenye manufaa ya moja kwa moja kwenye maisha yetu. Badala yake tumekijikita katika kusoma kwa nguvu zote mambo ambayo hayana faida kubwa kwetu.

Kuthibitisha hilo fuatilia kwa karibu ni taarifaa gani zinazofuatiliwa na vijana wengi kwenye magazeti, kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii na vyazo vingine vya habari. Kimsingi utakuta habari za udaku, michezo, burudani na vichekesho vikichukua nafasi kubwa na kupata wafuatiliaji wengi ambapo wengi wao ni vijana. Simaanishi kwamba hatutakiwi kufuatilia taarifa za kijamii hapana, bali tunatakiwa kuifahamu vizuri sana jamii yetu kwa kusoma taarifa na matukio ya kila siku yanayoendelea ili kuwa na uwezo wa kuishi kulingana na matukio yaliyopo kwenye jamii zetu.

Lakini pamoja na yote hayo kusoma mambo ya kutujenga fikra zetu ni muhimu zaidi na ndilo jambo litakalotuwezesha kuzikabili changamoto na matukio yote yanayojitokeza kwenye jamii zetu, hivyo tutajikuta tunazifahamu jamii zetu, matukio ndani ya jamii zetu, matatizo na changamoto zinazozikabili jamii zetu na mwisho kabisa tutakuja na suluhisho la matatizo na changamoto zinazoikabili jamii inayotuzunguka. Na kupitia suluhisho la matatizo na changamoto hizo itatupelekea kutengeneza fursa na kujipatia kipato…………………….

………………………………………….

Ndugu msomaji wangu, somo hili bado halijafika mwisho naweza kusema kuwa ndiyo kwanza limeanza, nitaendelea kukutumia makala fupi kupitia tovuti hii ili kukumbushana juu ya wajibu wetu kama vijana na nini tufanye ili kujikwamua na janga la umaskini, lakini ukitaka kuwa karibu na kufaidika zaidi na mafunzo unaweza kujiunga na kundi letu la WhatsApp (Vijana Tuamke) kupata masomo na semina mbalimbali.

Aidha tutajifunza ni namna gani tunaweza kuzitumia kurasa zetu mbali mbali za mitandao ya kijamii kama biashara na kuepuka yale mazoea ya kila siku kushinda kwenye mitandao ya kijamii na kutumia bando zetu wakati hali zetu zinaendelea kuwa ngumu sana kiuchumi. Hapa tutaangazia mitandao ya kijamii kama facebook, instagram, X(Zamani twitter), youtube n.k. Tutaangalia ni namna gani ya kufungua, kupangilia na kutumia kurasa hizo za mitandao ya kijamii kwa tija zaidi.

Elimu ya mtaani,Elimu ya fedha na uchumi

Pia kutakuwa na Ofa  ya Vitabu na maelekezo mbalimbali ya kitaalamu jinsi ya kuyageuza mazigira yanayotuzunguka kuwa fursa, namna ya kuvigeuza vyombo vyetu vya mawasiliano kuwa maduka yetu na kujitengenezea kipato. Kwenye group letu tuna masomo adimu na ya kipekee kabisa zaidi ya 100 ambayo huwezi kuyapata mahali pengine popote zaidi ya hapa. Masomo haya yanatoa mwanga mkubwa katika ufahamu wa suala zima la pesa, jinsi inavyozunguka kwenye biashara na hata saikolojia za watu na imani zao juu ya fedha na jinsi zinavyoathiri hali yao ya kiuchumi.

Kila somo jipya litafundishwa ndani ya mzunguko wa wiki mbili ambapo kwa wiki kutakuwa na siku tatu za masomo ambazo zitatangazwa kila linapotangazwa somo jipya. Aidha semina hizi zitakuwa za mara kwa mara zikijumuisha michanganuo/Business Plans bunifu kwa biashara zinazolipa Tanzania. Tutakuunga kwenye group letu kwa ada ndogo tu ya Tshs 10,000/=  kwa mzunguko wa wiki mbili.

Labda nikuambie kitu tu ndugu yangu msomaji, hautajutia kulipia Tshs 10,000/=  yako kwani kwa kusoma somo moja tu utakuwa tayari umefungua ubongo wako na tayari utaweza kuanza kutengeneza kipato chako kwa kuliweka somo moja tu kwenye vitendo. Hivyo unaweza kuamua kusoma somo moja tu kwanza kisha ukalifanyia kazi na baada ya kuona faida yake unaweza kuongeza masomo mengine zaidi kulingana na uhitaji wako.

Ni yangu matumaini kuwa tutakuwa pamoja kwenye masomo yetu yanayotarajia kuanza rasmi hivi karibuni. Tafadhali uonapo makala hii share na mwenzako unayempenda ili asipitwe na fursa hii adimu sanaa. Muhimu zaidi usikae mbali na tovuti yetu ili tunaporudi na taarifa rasmi ya somo letu la kwanza uwe wa kwanza kuipata maana tunaweza kutoa Ofa  maalumu kwa watu kadhaa watakaoanza kulipia ada ya kikundi.

MWISHO

Mwisho wa makala hii ndiyo mwanzo mzuri wa makala nyingine nyingi tu zitakazoangazia matumizi ya mitandao ya kijamii, namna gani tunaweza kuigeuza mitandao hiyo kuwa fursa ya kutuingizia kipato badala ya kupoteza muda huko na kujikuta tunapoteza mwelekeo wa kuzifikia ndoto zetu kwa sababu ya matumizi mabovu ya muda ndani ya mitandao ya kijamii.

Naitwa
Uncle J
(Jafari Ilyasa Kazohela)
Kwa maoni, maswali, mawasiliano zaidi pamoja na kutembelea kurasa zangu za mitandao ya kijamii:-

Tafadhali Gusa kitufe cha Whatsapp hapo chini:-

Au

Nipigie moja kwa moja kwa kugusa hapo chini:-

Au

Nitumie barua pepe
hapo chini:-

Au tembelea kurasa zangu za mitandao ya kijamii/Social Media Pages & Channels
hapo chini:-